9Mpenzi wangu, ninakufananisha na farasi jike aliyefungwa katika mojawapo ya magari ya vita ya Farao.
10Mashavu yako yanapendeza yakiwa na vipuli, shingo yako ikiwa na mikufu ya vito.
11Tutakufanyia vipuli vya dhahabu, vyenye kupambwa kwa fedha.
12Wakati mfalme alipokuwa mezani pake, manukato yangu yalisambaza harufu yake nzuri.
13Mpenzi wangu kwangu mimi ni kifuko cha manemane kati ya matiti yangu.