11Katika siku hiyo kilio kitakuwa kikubwa Yerusalemu, kama kilio cha Hadad-Rimoni katika tambarare ya Megido.
12Nchi itaomboleza, kila ukoo peke yake, nao wake zao peke yao. Ukoo wa nyumba ya Daudi na wake zao, ukoo wa nyumba ya Nathani na wake zao,
13ukoo wa nyumba ya Lawi na wake zao, ukoo wa Shimei na wake zao,
14na koo zote zilizobaki na wake zao.