9Mwimbieni yeye, mwimbieni yeye sifa; waambieni matendo yake yote ya ajabu.
10Lishangilieni jina lake takatifu; mioyo ya wale wamtafutao Bwana na ifurahi.
11Mtafuteni Bwana na nguvu zake; utafuteni uso wake siku zote.
12Kumbuka matendo ya ajabu aliyoyafanya, miujiza yake na hukumu alizozitamka,
13enyi wazao wa Israeli mtumishi wake, enyi wana wa Yakobo, wateule wake.