10Lishangilieni jina lake takatifu; mioyo ya wale wamtafutao Bwana na ifurahi.
11Mtafuteni Bwana na nguvu zake; utafuteni uso wake siku zote.
12Kumbuka matendo ya ajabu aliyoyafanya, miujiza yake na hukumu alizozitamka,
13enyi wazao wa Israeli mtumishi wake, enyi wana wa Yakobo, wateule wake.
14Yeye ndiye Bwana Mungu wetu; hukumu zake zimo duniani pote.