12Kumbuka matendo ya ajabu aliyoyafanya, miujiza yake na hukumu alizozitamka,
13enyi wazao wa Israeli mtumishi wake, enyi wana wa Yakobo, wateule wake.
14Yeye ndiye Bwana Mungu wetu; hukumu zake zimo duniani pote.
15Hulikumbuka agano lake milele, neno ambalo aliamuru, kwa vizazi elfu,
16agano alilolifanya na Abrahamu, kiapo alichomwapia Isaki.