13enyi wazao wa Israeli mtumishi wake, enyi wana wa Yakobo, wateule wake.
14Yeye ndiye Bwana Mungu wetu; hukumu zake zimo duniani pote.
15Hulikumbuka agano lake milele, neno ambalo aliamuru, kwa vizazi elfu,
16agano alilolifanya na Abrahamu, kiapo alichomwapia Isaki.
17Alilithibitisha kwa Yakobo kuwa amri, kwa Israeli liwe agano la milele: