18“Nitakupa wewe nchi ya Kanaani kuwa sehemu utakayoirithi.”
19Walipokuwa wachache kwa idadi, wachache sana na wageni ndani yake,
20walitangatanga kutoka taifa moja hadi jingine, kutoka ufalme mmoja hadi mwingine.
21Hakuruhusu mtu yeyote awaonee; kwa ajili yao aliwakemea wafalme, akisema:
22“Msiwaguse niliowatia mafuta; msiwadhuru manabii wangu.”