20walitangatanga kutoka taifa moja hadi jingine, kutoka ufalme mmoja hadi mwingine.
21Hakuruhusu mtu yeyote awaonee; kwa ajili yao aliwakemea wafalme, akisema:
22“Msiwaguse niliowatia mafuta; msiwadhuru manabii wangu.”
23Mwimbieni Bwana dunia yote; tangazeni wokovu wake siku baada ya siku.
24Tangazeni utukufu wake katikati ya mataifa, matendo yake ya ajabu miongoni mwa mataifa yote.