19Wana wa Hebroni walikuwa: Yeria alikuwa wa kwanza, wa pili Amaria, wa tatu Yahazieli, na wa nne Yekameamu.
20Wana wa Uzieli walikuwa: Mika wa kwanza na Ishia wa pili.
21Wana wa Merari walikuwa: Mahli na Mushi. Wana wa Mahli walikuwa: Eleazari na Kishi.
22Eleazari akafa bila ya kuwa na wana: alikuwa na binti tu. Binamu zao, wana wa Kishi, wakawaoa.
23Wana wa Mushi: Mahli, Ederi na Yeremothi; wote walikuwa watatu.