5na 4,000 watakuwa mabawabu, na wengine 4,000 watamsifu Bwana kwa ala za uimbaji nilizotoa kwa ajili ya kusudi hilo.”
6Daudi akawagawa Walawi katika makundi kufuatana na wana wa Lawi: Gershoni, Kohathi na Merari.
7Wana wa Wagershoni walikuwa wawili: Ladani na Shimei.
8Wana wa Ladani walikuwa watatu: Yehieli wa kwanza, Zethamu na Yoeli.
9Wana wa Shimei walikuwa watatu: Shelomothi, Hazieli na Harani. Hawa watatu walikuwa viongozi wa jamaa za Ladani.