1 Wakorintho 12

Je, wote ni mitume? Je, wote ni manabii? Je, wote ni walimu? Je, wote wanatenda miujiza?

1 Corinthians 12:29 (UKJV) Are all apostles? are all prophets? are all teachers? are all workers of miracles?

27Sasa ninyi ni mwili wa Kristo na kila mmoja wenu ni sehemu ya huo mwili.

28Mungu ameweka katika kanisa, kwanza mitume, pili manabii, tatu walimu, kisha watenda miujiza, pia karama za kuponya, karama za kusaidiana, karama za uongozi, aina mbalimbali za lugha.

29Je, wote ni mitume? Je, wote ni manabii? Je, wote ni walimu? Je, wote wanatenda miujiza?

30Je, wote wana karama ya kuponya? Je, wote hunena kwa lugha mpya? Je, wote wanatafsiri?

31Basi tamanini sana karama zilizo kuu. Nami nitawaonyesha njia iliyo bora zaidi.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.