1 Samweli 2

Wale waliokuwa na chakula tele wamejikodisha wenyewe ili kupata chakula, lakini wale waliokuwa na njaa hawana njaa tena. Mwanamke yule aliyekuwa tasa amezaa watoto saba, lakini yule ambaye alikuwa na wana wengi amedhoofika.

1 Samuel 2:5 (UKJV) They that were full have hired out themselves for bread; and they that were hungry ceased: so that the barren has born seven; and she that has many children is waxed feeble.

3“Msiendelee kusema kwa kiburi hivyo wala msiache vinywa vyenu kunena kwa kiburi, kwa kuwa Bwana ndiye Mungu ajuaye, na kwa yeye matendo hupimwa.

4“Pinde za mashujaa zimevunjika, lakini wale wanaojikwaa wamevikwa nguvu.

5Wale waliokuwa na chakula tele wamejikodisha wenyewe ili kupata chakula, lakini wale waliokuwa na njaa hawana njaa tena. Mwanamke yule aliyekuwa tasa amezaa watoto saba, lakini yule ambaye alikuwa na wana wengi amedhoofika.

6“Bwana huua na huleta uhai, hushusha chini mpaka kaburini na hufufua.

7Bwana humfanya mtu maskini naye hutajirisha, hushusha na hukweza.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.