1 Samweli 30

Daudi akafanya hili liwe amri na agizo kwa Israeli kutoka siku ile hata leo.

1 Samuel 30:25 (UKJV) And it was so from that day forward, that he made it a statute and an ordinance for Israel unto this day.

23Daudi akajibu, “La hasha, ndugu zangu, kamwe hamwezi kufanya hivyo kwa kile ambacho Bwana ametupatia. Yeye ametulinda na kuweka mikononi mwetu majeshi yale yaliyokuja kupigana dhidi yetu.

24Ni nani atasikiliza yale mnayosema? Fungu la mtu aliyekaa na vyombo litakuwa sawa na la yule aliyekwenda vitani. Wote watashiriki sawa.”

25Daudi akafanya hili liwe amri na agizo kwa Israeli kutoka siku ile hata leo.

26Daudi alipofika Siklagi, akatuma baadhi ya nyara kwa wazee wa Yuda, waliokuwa rafiki zake, akasema, “Tazama, hapa kuna zawadi kwa ajili yenu kutoka nyara za adui za Bwana.”

27Akazituma kwa wale waliokuwa Betheli, Ramoth-Negebu na Yatiri;

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.