15Aliipiga mishale na kutawanya adui, umeme wa radi na kuwafukuza.
16Mabonde ya bahari yalifunuliwa, na misingi ya dunia ikawa wazi kwa kukaripia kwake Bwana, kwa uvumi wa pumzi kutoka puani mwake.
17“Alinyoosha mkono kutoka juu na kunishika; alinitoa kutoka kilindi cha maji makuu.
18Aliniokoa kutoka adui wangu mwenye nguvu nyingi, kutoka adui zangu waliokuwa na nguvu nyingi kuliko mimi.
19Walinikabili siku ya msiba wangu, lakini Bwana alikuwa msaada wangu.