32Kwa maana ni nani aliye Mungu zaidi ya Bwana? Ni nani aliye Mwamba isipokuwa Mungu wetu?
33Mungu ndiye anivikaye nguvu na kufanya njia yangu kuwa kamilifu.
34Huifanya miguu yangu kama miguu ya kulungu, huniwezesha kusimama mahali palipo juu.
35Huifundisha mikono yangu kupigana vita; mikono yangu inaweza kupinda upinde wa shaba.
36Hunipa ngao yako ya ushindi, unajishusha chini ili kuniinua.