2 Samweli 22

Ninamwita Bwana, anayestahili kusifiwa, nami ninaokolewa kutoka kwa adui zangu.

2 Samuel 22:4 (UKJV) I will call on the LORD, who is worthy to be praised: so shall I be saved from mine enemies.

2Akasema: “Bwana ni mwamba wangu, ngome yangu na mwokozi wangu,

3Mungu wangu ni mwamba wangu, ambaye kwake ninakimbilia, ngao yangu na pembe ya wokovu wangu. Yeye ni ngome yangu, kimbilio langu na mwokozi wangu, huniokoa kutoka kwa watu wenye jeuri.

4Ninamwita Bwana, anayestahili kusifiwa, nami ninaokolewa kutoka kwa adui zangu.

5“Mawimbi ya mauti yalinizunguka, mafuriko ya maangamizi yalinilemea.

6Kamba za kuzimu zilinizunguka, mitego ya mauti ilinikabili.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.