4Ninamwita Bwana, anayestahili kusifiwa, nami ninaokolewa kutoka kwa adui zangu.
5“Mawimbi ya mauti yalinizunguka, mafuriko ya maangamizi yalinilemea.
6Kamba za kuzimu zilinizunguka, mitego ya mauti ilinikabili.
7Katika shida yangu nalimwita Bwana, nilimlilia Mungu wangu. Kutoka Hekaluni mwake alisikia sauti yangu, kilio changu kikafika masikioni mwake.
8“Dunia ilitetemeka na kutikisika, misingi ya mbingu ikatikisika, vilitetemeka kwa sababu alikuwa amekasirika.