12Ndani yake walikuwepo aina zote za wanyama wenye miguu minne, nao watambaao nchini, na ndege wa angani.
13Ndipo sauti ikamwambia “Petro, ondoka, uchinje na ule.”
14Petro akajibu, “La hasha Bwana! Sijawahi kamwe kula kitu chochote kilicho najisi.”
15Ile sauti ikasema naye mara ya pili, “Usikiite najisi kitu chochote Mungu alichokitakasa.”
16Jambo hili lilitokea mara tatu na ghafula ile nguo ikarudishwa mbinguni.