15Hata hivyo, kama hutamtii Bwana Mungu wako na kuzishika kwa bidii amri zake zote na maagizo ninayokupa leo, laana hizi zote zitakuja juu yako na kukupata:
16Utalaaniwa mjini na utalaaniwa mashambani.
17Kapu lako na chombo chako cha kukandia kitalaaniwa.
18Uzao wa tumbo lako utalaaniwa, mazao ya ardhi yako, ndama wa makundi yako ya ngʼombe na wana-kondoo wa makundi yako.
19Utalaaniwa uingiapo na utokapo.