25Lakini sasa kwa kuwa ile imani imekuja, hatusimamiwi tena na sheria.
26Kwa maana ninyi nyote mmekuwa watoto wa Mungu katika Kristo Yesu kwa njia ya imani.
27Kwa maana wote mliobatizwa ndani ya Kristo, mmemvaa Kristo.
28Wala hakuna tena Myahudi au Myunani, mtumwa au mtu huru, mwanaume wala mwanamke, maana nyote mmekuwa wamoja ndani ya Kristo Yesu.
29Nanyi mkiwa ni mali ya Kristo, basi ninyi ni wa uzao wa Abrahamu na warithi sawasawa na ile ahadi.