1Abramu alipokuwa na miaka tisini na tisa, Bwana akamtokea akamwambia, “Mimi ndimi Mungu Mwenyezi; enenda mbele zangu na uishi kwa unyofu.
2Nami nitafanya Agano langu kati yangu na wewe, nami nitakuzidisha sana sana.”
3Abramu akaanguka kifudifudi, naye Mungu akamwambia,
4“Kwa upande wangu, hili ndilo Agano langu na wewe: Wewe utakuwa baba wa mataifa mengi.