2Nami nitafanya Agano langu kati yangu na wewe, nami nitakuzidisha sana sana.”
3Abramu akaanguka kifudifudi, naye Mungu akamwambia,
4“Kwa upande wangu, hili ndilo Agano langu na wewe: Wewe utakuwa baba wa mataifa mengi.
5Jina lako hutaitwa tena Abramu, bali jina lako litakuwa Abrahamu, kwa maana nimekufanya wewe baba wa mataifa mengi.
6Nitakufanya uwe na uzao mwingi sana, kwako yatatoka mataifa nao wafalme watatoka kwako.