Mwanzo 3

Adamu akamwita mkewe Eva, kwa kuwa atakuwa mama wa wote walio hai.

Genesis 3:20 (UKJV) And Adam called his wife's name Eve; because she was the mother of all living.

18Itazaa miiba na mibaruti kwa ajili yako, nawe utakula mimea ya shambani.

19Kwa jasho la uso wako utakula chakula chako hadi utakaporudi ardhini, kwa kuwa ulitwaliwa kutoka humo, kwa kuwa wewe u mavumbi na mavumbini wewe utarudi.”

20Adamu akamwita mkewe Eva, kwa kuwa atakuwa mama wa wote walio hai.

21Bwana Mungu akawatengenezea Adamu na mkewe mavazi ya ngozi, akawavika.

22Kisha Bwana Mungu akasema, “Sasa mtu huyu amekuwa kama mmoja wetu, kwa kujua mema na mabaya. Sharti asiruhusiwe kunyoosha mkono wake na kuchuma pia kutoka mti wa uzima akala, naye akaishi milele.”

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.