Mwanzo 30

Ndipo Mungu akamkumbuka Raheli, akasikia maombi yake na akafungua tumbo lake.

Genesis 30:22 (UKJV) And God remembered Rachel, and God hearkened to her, and opened her womb.

20Ndipo Lea aliposema, “Mungu amenizawadia kwa zawadi ya thamani sana. Wakati huu mume wangu ataniheshimu kwa sababu nimemzalia wana sita.” Kwa hiyo akamwita Zabuloni.

21Baadaye akamzaa mtoto wa kike akamwita Dina.

22Ndipo Mungu akamkumbuka Raheli, akasikia maombi yake na akafungua tumbo lake.

23Akapata mimba na akamzaa mwana na kusema, “Mungu ameniondolea aibu yangu.”

24Akamwita Yosefu na kusema, “Bwana na anipe mwana mwingine.”

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.