44Njoo sasa na tufanye agano, wewe na mimi, na liwe kama shahidi kati yetu.”
45Hivyo Yakobo akachukua jiwe, akalisimamisha kama nguzo.
46Akawaambia jamaa yake, “Kusanyeni mawe.” Hivyo wakachukua mawe na kuyakusanya yakawa lundo, wakala chakula hapo karibu na hilo lundo.
47Labani akaliita Yegar-Sahadutha na Yakobo akaliita Galeedi.
48Labani akasema, “Lundo hili ni shahidi kati yako na mimi leo.” Ndiyo maana likaitwa Galeedi.