Mwanzo 31

Labani akaliita Yegar-Sahadutha na Yakobo akaliita Galeedi.

Genesis 31:47 (UKJV) And Laban called it Jegarsahadutha: but Jacob called it Galeed.

45Hivyo Yakobo akachukua jiwe, akalisimamisha kama nguzo.

46Akawaambia jamaa yake, “Kusanyeni mawe.” Hivyo wakachukua mawe na kuyakusanya yakawa lundo, wakala chakula hapo karibu na hilo lundo.

47Labani akaliita Yegar-Sahadutha na Yakobo akaliita Galeedi.

48Labani akasema, “Lundo hili ni shahidi kati yako na mimi leo.” Ndiyo maana likaitwa Galeedi.

49Pia liliitwa Mispa, kwa sababu alisema, “Bwana na aweke ulinzi kati yako na mimi wakati kila mmoja akiwa mbali na mwingine.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.