7Mali zao zilikuwa nyingi sana kiasi kwamba haikuwa rahisi wao kuishi pamoja, nchi waliyokuwa wakiishi isingewatosha wote kwa ajili ya mifugo yao.
8Kwa hiyo Esau (ambaye ni Edomu) aliishi katika nchi ya kilima huko Seiri.
9Hawa ndio wazao wa Esau, baba wa Waedomu, katika nchi ya kilima cha Seiri.
10Haya ndiyo majina ya wana wa Esau: Elifazi, mwana wa Esau ambaye mkewe Ada alimzalia; na Reueli, mwana wa Esau ambaye mkewe Basemathi alimzalia.
11Wana wa Elifazi ni: Temani, Omari, Sefo, Gatamu na Kenazi.