11Kila kuhani husimama siku kwa siku akifanya huduma yake ya ibada, na kutoa tena na tena dhabihu zile zile ambazo haziwezi kamwe kuondoa dhambi.
12Lakini huyu kuhani akiisha kutoa dhabihu moja kwa ajili ya dhambi kwa wakati wote, aliketi mkono wa kuume wa Mungu.
13Tangu wakati huo anangoja mpaka adui zake wawekwe chini ya miguu yake,
14kwa sababu kwa dhabihu moja amewafanya kuwa wakamilifu milele wale wote wanaotakaswa.
15Pia Roho Mtakatifu anatushuhudia kuhusu jambo hili. Kwanza anasema: