Hosea 13

Hivyo katika hasira yangu nilikupa mfalme na katika ghadhabu yangu nilimwondoa.

Hosea 13:11 (UKJV) I gave you a king in mine anger, and took him away in my wrath.

9“Ee Israeli, umeangamizwa, kwa sababu wewe u kinyume nami, kinyume na msaidizi wako.

10Yuko wapi mfalme wako, ili apate kukuokoa? Wako wapi watawala wako katika miji yako yote ambao ulisema kuwahusu, ‘Nipe mfalme na wakuu’?

11Hivyo katika hasira yangu nilikupa mfalme na katika ghadhabu yangu nilimwondoa.

12Kosa la Efraimu limehifadhiwa, dhambi zake zimewekwa katika kumbukumbu.

13Utungu kama wa mwanamke anayejifungua mtoto humjia, lakini yeye ni mtoto asiyekuwa na hekima; wakati utakapowadia hatatoka katika tumbo la mama yake.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.