Hosea 13

Niliwatunza huko jangwani, katika nchi yenye joto liunguzalo.

Hosea 13:5 (UKJV) I did know you in the wilderness, in the land of great drought.

3Kwa hiyo watakuwa kama ukungu wa asubuhi, kama umande wa alfajiri utowekao, kama makapi yapeperushwayo kutoka sakafu ya kupuria nafaka, kama moshi utorokao kupitia dirishani.

4“Bali mimi ndimi Bwana Mungu wenu, niliyewaleta ninyi toka Misri. Msimkubali Mungu mwingine ila mimi, hakuna Mwokozi isipokuwa mimi.

5Niliwatunza huko jangwani, katika nchi yenye joto liunguzalo.

6Nilipowalisha, walishiba, waliposhiba, wakajivuna, kisha wakanisahau mimi.

7Kwa hiyo nitakuja juu yao kama simba, kama chui nitawavizia kando ya njia.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.