4“Bali mimi ndimi Bwana Mungu wenu, niliyewaleta ninyi toka Misri. Msimkubali Mungu mwingine ila mimi, hakuna Mwokozi isipokuwa mimi.
5Niliwatunza huko jangwani, katika nchi yenye joto liunguzalo.
6Nilipowalisha, walishiba, waliposhiba, wakajivuna, kisha wakanisahau mimi.
7Kwa hiyo nitakuja juu yao kama simba, kama chui nitawavizia kando ya njia.
8Kama dubu aliyenyangʼanywa watoto wake, nitawashambulia na kurarua vifua vyenu. Kama simba nitawala; mnyama pori atawararua vipande vipande.