16Waisraeli ni wakaidi, kama mtamba wa ngʼombe ambaye ni mkaidi. Ni jinsi gani basi Bwana anaweza kuwachunga kama wana-kondoo katika shamba la majani?
17Efraimu amejiunga na sanamu, ondokana naye!
18Hata wakati wamemaliza vileo vyao wanaendelea na ukahaba wao, watawala wao hupenda sana njia za aibu.
19Kisulisuli kitawafagilia mbali na dhabihu zao zitawaletea aibu.