1Tazama sasa, Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote, yu karibu kuwaondolea Yerusalemu na Yuda upatikanaji wa mahitaji na misaada, upatikanaji wote wa chakula na tegemeo lote la maji,
2shujaa na mtu wa vita, mwamuzi na nabii, mwaguzi na mzee,
3jemadari wa kikosi cha watu hamsini na mtu mwenye cheo, mshauri, fundi stadi na mlozi mjanja.
4Nitawafanya wavulana wawe maafisa wao, watoto ndio watakaowatawala.