9Kumbuka kuwa ulinifinyanga kama udongo wa mfinyanzi. Je, sasa utanifanya kuwa mavumbi tena?
10Je, wewe hukunimimina mimi kama maziwa, na kunigandisha kama jibini,
11ukanivika ngozi na nyama, na kuniunga pamoja kwa mifupa na mishipa?
12Umenipa uhai na kunitendea wema, katika uangalizi wako umeilinda roho yangu.
13“Lakini hili ndilo ulilolificha moyoni mwako, nami ninajua kuwa hili lilikuwa katika nia yako: