11ukanivika ngozi na nyama, na kuniunga pamoja kwa mifupa na mishipa?
12Umenipa uhai na kunitendea wema, katika uangalizi wako umeilinda roho yangu.
13“Lakini hili ndilo ulilolificha moyoni mwako, nami ninajua kuwa hili lilikuwa katika nia yako:
14Kama nilifanya dhambi, ungekuwa umeniona, wala usingeacha kosa langu lipite bila kuadhibiwa.
15Kama nina hatia, ole wangu! Hata kama ningekuwa sina hatia, siwezi kukiinua kichwa changu, kwa kuwa nimejawa na aibu, na kuzama katika mateso yangu.