1“Nayachukia sana haya maisha yangu; kwa hiyo nitatoa malalamiko yangu kwa wazi bila kujizuia, nami nitanena kutokana na uchungu wa moyo wangu.
2Nitamwambia Mungu: Usinihukumu, bali niambie una mashtaka gani dhidi yangu.
3Je, inakupendeza wewe kunionea, kuikataa kwa dharau kazi ya mikono yako, huku wewe ukitabasamu juu ya mipango ya waovu?
4Je, wewe una macho ya kimwili? Je, wewe huona kama mwanadamu aonavyo?