Ayubu 11

Unamwambia Mungu, ‘Imani yangu ni kamili nami ni safi mbele zako.’

Job 11:4 (UKJV) For you have said, My doctrine is pure, and I am clean in yours eyes.

2“Je, maneno haya yote yapite bila kujibiwa? Je, huyu mnenaji athibitishwe kuwa na haki?

3Je, maneno yako ya upuzi yawafanye watu wanyamaze kimya? Je, mtu asikukemee unapofanya dhihaka?

4Unamwambia Mungu, ‘Imani yangu ni kamili nami ni safi mbele zako.’

5Aha! Laiti kwamba Mungu angesema, kwamba angefungua midomo yake dhidi yako,

6naye akufunulie siri za hekima, kwa kuwa hekima ya kweli ina pande mbili. Ujue hili: Mungu amesahau hata baadhi ya dhambi zako.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.