4Unamwambia Mungu, ‘Imani yangu ni kamili nami ni safi mbele zako.’
5Aha! Laiti kwamba Mungu angesema, kwamba angefungua midomo yake dhidi yako,
6naye akufunulie siri za hekima, kwa kuwa hekima ya kweli ina pande mbili. Ujue hili: Mungu amesahau hata baadhi ya dhambi zako.
7“Je, waweza kujua siri za Mungu? Je, waweza kuyachunguza mambo yote kumhusu Mwenyezi?
8Ni juu mno kuliko mbingu: waweza kufanya nini? Kina chake ni kirefu kuliko kuzimu: wewe waweza kujua nini?