5Aha! Laiti kwamba Mungu angesema, kwamba angefungua midomo yake dhidi yako,
6naye akufunulie siri za hekima, kwa kuwa hekima ya kweli ina pande mbili. Ujue hili: Mungu amesahau hata baadhi ya dhambi zako.
7“Je, waweza kujua siri za Mungu? Je, waweza kuyachunguza mambo yote kumhusu Mwenyezi?
8Ni juu mno kuliko mbingu: waweza kufanya nini? Kina chake ni kirefu kuliko kuzimu: wewe waweza kujua nini?
9Kipimo chake ni kirefu kuliko dunia, nacho ni kipana kuliko bahari.