20Hunyamazisha midomo ya washauri wanaoaminika, na kuondoa busara ya wazee.
21Huwamwagia dharau wanaoheshimika, na kuwavua silaha wenye nguvu.
22Hufunua mambo ya ndani ya gizani, na kuyaleta nuruni yale yaliyositirika sana.
23Huyafanya mataifa yatukuke na kuyaangamiza; hufanya mataifa kuwa makubwa, naye huyatawanya.
24Huwaondolea viongozi wa nchi akili zao; huwapeleka watangetange nyikani pasipo na njia.