17Sikilizeni maneno yangu kwa makini; nayo masikio yenu yaingize kile nisemacho.
18Sasa kwamba nimekwisha kutayarisha mambo yangu, ninajua mimi nitahesabiwa kuwa na haki.
19Je, kuna yeyote anayeweza kuleta mashtaka dhidi yangu? Kama ndivyo, nitanyamaza kimya na nife.
20“Ee Mungu, unijalie tu mimi haya mambo mawili, nami sitajificha uso wako:
21Ondoa mkono wako uwe mbali nami, nawe uache kuniogofya kwa hofu zako kuu.