15Moto utakaa katika hema lake; moto wa kiberiti utamwagwa juu ya makao yake.
16Mizizi yake chini itakauka na matawi yake juu yatanyauka.
17Kumbukumbu lake litatoweka katika dunia, wala hatakuwa na jina katika nchi.
18Ameondolewa nuruni na kusukumiwa gizani, naye amefukuzwa mbali atoke duniani.
19Hana mtoto wala mzao miongoni mwa watu wake, wala aliyenusurika mahali alipoishi.