6Mwanga hemani mwake umekuwa giza; taa iliyo karibu naye imezimika.
7Nguvu za hatua zake zimedhoofishwa; shauri lake baya litamwangusha.
8Miguu yake imemsukumia kwenye wavu, naye anatangatanga kwenye matundu ya wavu.
9Tanzi litamkamata kwenye kisigino; mtego utamshikilia kwa nguvu.
10Kitanzi kimefichwa ardhini kwa ajili yake; mtego uko kwenye njia yake.