4Wewe unayejirarua mwenyewe vipande vipande katika hasira yako, je, dunia iachwe kwa ajili yako wewe? Au ni lazima miamba iondolewe mahali pake?
5“Taa ya mwovu imezimwa, nao mwali wa moto wake umezimika.
6Mwanga hemani mwake umekuwa giza; taa iliyo karibu naye imezimika.
7Nguvu za hatua zake zimedhoofishwa; shauri lake baya litamwangusha.
8Miguu yake imemsukumia kwenye wavu, naye anatangatanga kwenye matundu ya wavu.