5“Taa ya mwovu imezimwa, nao mwali wa moto wake umezimika.
6Mwanga hemani mwake umekuwa giza; taa iliyo karibu naye imezimika.
7Nguvu za hatua zake zimedhoofishwa; shauri lake baya litamwangusha.
8Miguu yake imemsukumia kwenye wavu, naye anatangatanga kwenye matundu ya wavu.
9Tanzi litamkamata kwenye kisigino; mtego utamshikilia kwa nguvu.