10Amenibomoa kila upande hadi nimeisha; amelingʼoa tegemeo langu kama mti.
11Hasira yake imewaka juu yangu; amenihesabu kuwa miongoni mwa adui zake.
12Majeshi yake yananisogelea kwa nguvu; yamenizingira, yamepiga kambi kulizunguka hema langu.
13“Amewatenga ndugu zangu mbali nami; wale tunaojuana nao wamefarakana nami kabisa.
14Watu wa jamaa yangu wamekwenda mbali; rafiki zangu wamenisahau.