15Wageni wangu na watumishi wangu wa kike wananiona kama mgeni; wananitazama kama mgeni.
16Namwita mtumishi wangu, wala haitiki, ingawa namwomba kwa kinywa changu mwenyewe.
17Pumzi ya kinywa changu ni kinyaa kwa mke wangu; nimekuwa chukizo mno kwa ndugu zangu mwenyewe.
18Hata watoto wadogo hunidhihaki; ninapojitokeza, hunifanyia mzaha.
19Rafiki zangu wa moyoni wote wananichukia kabisa; wale niwapendao wamekuwa kinyume nami.