11Nguvu za ujana zilizoijaza mifupa yake, zitalala naye mavumbini.
12“Ingawa uovu ni mtamu kinywani mwake naye huuficha chini ya ulimi wake,
13ingawa hawezi kukubali kuuachia uende, lakini huuweka kinywani mwake.
14Hata hivyo chakula chake kitakuwa kichungu tumboni mwake, nacho kitakuwa sumu kali ya nyoka ndani yake.
15Atatema mali alizozimeza; Mungu atalifanya tumbo lake kuzitapika.