13ingawa hawezi kukubali kuuachia uende, lakini huuweka kinywani mwake.
14Hata hivyo chakula chake kitakuwa kichungu tumboni mwake, nacho kitakuwa sumu kali ya nyoka ndani yake.
15Atatema mali alizozimeza; Mungu atalifanya tumbo lake kuzitapika.
16Atanyonya sumu za majoka; meno ya nyoka mwenye sumu kali yatamuua.
17Hatafurahia vijito, mito inayotiririsha asali na siagi.