Ayubu 20

Kama ndoto hutoweka, wala hapatikani tena, amefukuziwa mbali kama maono ya usiku.

Job 20:8 (UKJV) He shall fly away as a dream, and shall not be found: yea, he shall be chased away as a vision of the night.

6Ingawa kujikweza kwake hufikia mbinguni na kichwa chake hugusa mawingu,

7ataangamia milele kama mavi yake mwenyewe. Wale waliomwona watauliza, ‘Yuko wapi?’

8Kama ndoto hutoweka, wala hapatikani tena, amefukuziwa mbali kama maono ya usiku.

9Jicho lililomwona halitamwona tena; mahali pake hapatamwona tena.

10Watoto wake watalipa yote baba yao aliyowadhulumu maskini, nayo mikono yake itarudisha mali yote aliyonyangʼanya watu.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.